Timu hiyo ambayo imepanda daraja, inapambana kubaki katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara
Uongozi wa timu ya Tabora United, umeweka wazi unajivunia ujio wa nyota wao mpya, Emotan Cletus Eba, baada ya kuwasili leo nchini Tanzania kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.
Tabora United ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda daraja zikiwa zinapambana kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
18:00 - 28.01.2024
KANDANDA Simba SC, Yanga SC kurejea mzigoni wiki hii michuano ya ASFC
Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Jumanne na Jumatano baada ya mapumziko ya zaidi ya mwezi mmoja
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Tabora United, Chritina Mwagala, wachezaji wao wanafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwa kwenye ubora kitaifa na baadaye kimataifa.
“Emotan Cletus Eba, ni fundi halisi wa mpira kutoka Nigeria, ametua Tabora United,” amesema Mwagala.
16:00 - 22.01.2024
KANDANDA Bosi Simba SC aahidi kupunguza zaidi nyota wao
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya klabu hiyo kufanya Mkutano Mkuu wa kila mwaka ambapo baadhi ya wanachama walionesha kutofurahia usajili wa sasa
Amesema Eba, 23 ametokea timu ya Sunshine Stars inayoshiriki Ligi Kuu Nigeria ambapo amezaliwa mjini Ekong na amekuwa na uwezo mzuri wa kufunga na kutoa asisti ya mabao.
Pia Eba aliwahi kucheza katika timu ya Rivers United ambapo alicheza michezo mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
18:37 - 17.01.2024
KANDANDA Nahodha Singida FG atimkia Cape Town City ya Afrika Kusini
Mchezaji huyo ni Mtanzania Gadiel Michael ambaye aliwahi kuzichezea Azam, Yanga na Simba kwa nyakati tofauti
Katika msimamo wa ligi hiyo, Tabora United inashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 15 baada ya kucheza michezo 13, ikishinda mitatu, sare sita na kufungwa minne.