Simba SC yaitumia salamu Asec Mimosa

KANDANDA Simba SC yaitumia salamu Asec Mimosa

Na Zahoro Mlanzi • 18:00 - 19.11.2023

Timu hiyo kwa sasa ipo katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mimosa.

Katika kile kinachoonekana imetuma salama kwa Asec Mimosa ya Ivory Coast, timu ya Simba SC, imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dar City katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Mo Arena, Dar es Salaam.

Simba kwa sasa ipo katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mimosa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 25 Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba katika mchezo huo, yalifungwa Wacameroon, beki Che Malone Fondoh na kiungo mshambuliaji Leandre Willy Essomba Onana, beki mzawa Israel Patrick Mwenda na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri.

Katika mchezo huo ambao haukuwa na mashabiki wengi, Simba ilitawala kwa kiasi kikubwa na kufanya mashabiki wao kushangilia huku wakitaja jina la Asec Mimosa.

Hata hivyo, timu hiyo bado ipo chini ya Kocha wa Daniel Cadena ambaye anainoa kwa baada ya kutimuliwa kwa Roberto Oliviera 'Robertinho'.

Wakati huo huo, mchezaji wa timu hiyo, Mohamed Mussa, amefiwa na baba yake mzazi, Mussa Mzee Saleh aliyefariki dunia mapema visiwani Zanzíbar na anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo.

Tags: