Kocha Yanga aipania Al-Merreikh

KANDANDA Kocha Yanga aipania Al-Merreikh

Zahoro Mlanzi • 14:09 - 04.09.2023

Yanga itamenyana na Al-Merreikh ya Sudan Jumamosi Septemba 16.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia Argentina, amefuta mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo na kuingia kambini na kuanza maandalizi kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan.

Yanga ambao imeanza msimu huu kwa mafanikio kutokana na kutoa vipigo vizito katika Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa sasa wapo kwenye mapumziko ya wiki mbili kwa ajili ya kupisha michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa Afrika (Afcon) zinazotarajia kufanyika nchini Ivory Coast.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya kuwania kufuzu katika makundi ya michuano hiyo, Septemba 16, mwaka huu kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa Septemba 30, mwaka huu jijini Dar.

Akizungumza kuelekea maandalizi ya mchezo huo, Gamondi alisema haoni sababu ya kutoa mapunzukio kwa wachezaji wake kwani alishatoa mapumziko ya siku moja.

Alisema wapo katika kipindi kigumu cha kupisha michezo ya timu za taifa kutokana na ratiba ngumu iliyokuwepo mbele yao, hivyo hawawezi kupumzika.

“Hakuna sababu ya kupumzika, tayari tulipumzika siku moja na tayari turejea uwanjani, tunatakiwa kufikia malengo yetu hivyo ni vyema tukaongeza nguvu katika kipindi hiki kuhakikisha tunafikia malengo yetu,” alisema Gamondi.

Tags: