Kocha Mtibwa Sugar atimuliwa, Katwila anukia

© Kwa Hisani

KANDANDA Kocha Mtibwa Sugar atimuliwa, Katwila anukia

Zahoro Mlanzi • 21:13 - 18.10.2023

Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu tatu katika Ligi Kuu Bara ambazo hadi sasa hazijaonja ushindi wakiwa nafasi ya 15 na alama zao mbili baada ya mechi tano.

Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Manungu, Turiani, Morogoro, umeachana na Kocha wao, Habib Kondo baada kufundisha kwenye mechi tano za ligi.

Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu tatu katika Ligi Kuu Bara ambazo hadi sasa hazijaonja ushindi wakiwa nafasi ya 15 na alama zao mbili baada ya mechi tano.

Uamuzi wa kumfuta kazi Kondo umekuja siku moja kabla ya mchezo wao wa ligi ambao unachezwa kesho kwenye Uwanja wa Manungu dhidi ya Kagera Sugar.

"Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na Kocha wetu Habib Kondo na kuanzia sasa sio kocha katika kikosi chetu, tunamtakia kila la kheri," imesomeka taarifa ya Mtibwa iliyowekwa wazi kwa vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine, Kocha wa zamani wa Ihefu FC ya Mbeya, Zuber Katwila, anatajwa kuwa ndio mrithi wa Kondo ndani ya Mtibwa Sugar.

Licha ya kuwa Mtibwa Sugar wenyewe wamekataa kuthibitisha hilo lakini taarifa zinadai huenda kocha huyo akatambulishwa muda wowote kuanzia sasa.

Tags: