Ferreira afunguka kiwango cha Rupia

KANDANDA Ferreira afunguka kiwango cha Rupia

Zahoro Mlanzi • 19:52 - 02.11.2023

Ni mchezaji mgeni ndani ya timu lakini kwa jinsi anavyocheza, anavyoshirikiana na wenzake utadhani ana muda mrefu kikosini

Kocha wa timu ya Singida Fountain Gate FC, Ricardo Ferreira, amesema straika wake mpya, Mkenya Elvis Rupia akizoea Ligi Kuu Bara atakuwa msaada mkubwa kwa timu.

Singida FG imetoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Ihefu FC katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo, matokeo ambayo hayakufurahisha mashabiki wao.

Ferreira amesema walitawala mchezo na wachezaji wake walicheza vizuri ila anaamini watapata matokeo katika michezo inayofuata.

Amesema anafahamu presha iliyokuwa kwa mashabiki lakini kwa jinsi anavyoiona timu yake ni mchezaji mgeni ndani ya timu lakini kwa jinsi anavyocheza, anavyoshirikiana na wenzake utadhani ana muda mrefu kikosini matokeo.

"Nimeambia ni mchezaji mgeni ndani ya timu lakini kwa jinsi anavyocheza, anavyoshirikiana na wenzake utadhani ana muda mrefu kikosini," amesema Ferreira.

Ameongeza kama atapata muda mwingi wa kucheza na kuzoeana na wenzake atafunga mabao mengi zaidi.

Rupia alisajiliwa na Singida FG akitokea Polisi ya Kenya ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa akifunga zaidi ya mabao 25 katika msimu wa 2022/23. 

Fuatilia Pulse Sports Kenya kwenye WhatsApp kwa habari zaidi.

Tags: